MATUMIZI YA POMBE, TUMBAKU YAMEPUNGUA NCHINI

Serikali kupitia Wizara ya Afya, imesema matumizi ya Pombe yamepungua kutoka asilimia 29.3 mwaka 2012 hadi asilimia 20 mwaka 2023, huku matumizi ya Tumbaku yakipungua kutoka asilimia 14.1 mwaka 2012 hadi asilimia 10 mwaka 2023.

Hayo yamebainishwa hii leo Juni 2, 2025 Bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Jenista Mhagama huku akisema kati ya Julai 2024 hadi Machi 2025, pia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ilitoa msamaha wa shilingi bilioni 10.64 kwa wagonjwa 42,714 walioshindwa kumudu gharama za matibabu.

Kuhusu huduma zinazoongoza kutolewa msamaha Mhagama amesema ni usafishaji damu, wagonjwa mahututi (ICU), vipimo vya CT Scan na MRI pamoja na dawa.

Aidha, amesema utafiti uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) mwaka 2024 umebaini ugonjwa wa kisukari katika jamii umepungua kutoka asilimia 9.1 mwaka 2012 hadi asilimia 2.9 mwaka 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *