Mataifa matatu ya Afrika Magharibi amabyoni Mali, Burkina Faso na Niger yamejiondoa kwenye shirika la kiuchumi la kieneo la ECOWAS, Wamesema viongozu wao wa kijeshi, jana Jumapili.

Wote wamelaumu ECOWAS kwa hatua kandamizi za kuwawekea vikwazo, kama njia ya kuwalazimisha kuachana na mapinduzi yaliofanyika kwenye mataifa yao. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, ECOWAS kupitia taarifa imesema kwamba haijafahamishwa rasmi kuhusu uamuzi wa mataifa hayo.