Mashabiki Wote Wa Arsenal Wahamia Tottenham

Na Ibrahim Rojala

Mashabiki wa Arsenal wanaomba muujiza wa kipekee utokee usiku wa Jumanne ya leo wakati Tottenham Hotspur watakapoalika Manchester City kwa mechi muhimu zaidi kwao kuliko hata Tottenham wenyewe kwakuwa ni mechi itakayoamua nani atakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) inayotarajiwa kukamilika wikendi ijayo.

Man-City wanakwenda Tottenham, katika uwanja wa Tottenham Hotspur Stadium jijini London wakijua kuwa ni lazima washinde mchezo huo wa kiporo ili kuipiku Arsenal kileleni kabla mechi za raundi ya mwisho Jumapili ijayo.

Arsenal ilirejea tena kileleni mwa Ligi kuu Uingereza baada ya kuibonda   Manchester United goli 1-0 Jumapili ya Mei 12,2024 kupitia goli la mshambuliaji Leandro Trossard dakika ya 20 ambalo lilitosha kuwapa Gunners ushindi katika uwanja wa Old Trafford na kurejea katika nafasi ya kwanza wakiwa na alama 86, moja mbele ya Man-City (85) walio na mechi moja kibindoni ambayo wanakwenda kuikamilisha hii leo.

Man-City inaingia uwanjani leo ikiwa na kazi mbili,moja kupata alama tatu muhimu na pili kutaka kuweka rekodi ya kubeba ubingwa wa EPL mara nne mfululizo na hili litawezekana iwapo ikishinda mchezo wa leo na kushinda katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Wes Ham United Jumapili ijayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *