Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega amesema katika mwaka 2023/2024, idadi ya mifugo nchini imeongezeka kutoka ng’ombe milioni 36.6 hadi ng’ombe milioni 37.9, mbuzi kutoka milioni 26.6 hadi milioni 27.6, na kondoo kutoa milioni 9.1 hadi milioni 9.4.
Ameyasema hayo hii leo Mei 14,2024 kupitia hotuba ya mpango na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara ya mifugo na uvuvikwa mwaka 2024/2025 ambapo amebainisha kuwapi kuku wameongezeka kutoka milioni 97.9 hadi milioni 103.1 ambapo kuku wa asili wameongezeka kutoka milioni 45.1 hadi milioni 47.4, kuku wa kisasa wameongezeka kutoka milioni 52.9 hadi milioni 55.7 na nguruwe wameongezeka kutoka milioni 3.7 hadi milioni 3.9.
Aidha, Sekta ya Mifugo kwa mwaka 2022 ilikua kwa asilimia 5 na kuchangia asilimia 6.7 kwenye Pato la Taifa hadi kufikia Aprili, 2024, jumla ya ng’ombe 2,957,724 na mbuzi na kondoo 2,828,248 wenye thamani ya Shilingi trilioni 3.4, waliuzwa katika minada mbalimbali hapa nchini ikilinganishwa na ng’ombe 2,218,293 na mbuzi na kondoo 2,121,187 waliokuwa na thamani ya Shilingi trilioni 1.7 waliouzwa katika mwaka 2022/2023. Ongezeko la idadi ya mifugo iliyouzwa minadani limetokana na kuongezeka kwa mahitaji ya nyama katika soko la ndani na nje ya nchi pamoja na hamasa ya uvunaji wa mifugo.
Aidha uzalishaji wa nyama umeongezeka kutoka tani 803,264.3 (mwaka 2022/2023), hadi tani 963,856.55 (mwaka 2023/2024), ikiwa ni sawa na ongezeko la asimilia 16.7, kati ya hizo, nyama ya ng’ombe tani 612,808.50; mbuzi tani 134,403.35, kondoo tani 28,290.00; kuku tani 132,442.28, na nguruwe tani 55,912.42 kwa mwaka 2023/2024 ikilinganishwa na nyama ya ng’ombe tani 544,983.8; mbuzi tani 91,893.8; kondoo tani 21,888.05; kuku tani 96,915.6 na nguruwe tani 47,583.1 kwa mwaka 2022/2023.
Ongezeko lililoelezwa kuwa limechangiwa na wafugaji kuhamasika kuvuna mifugo yao na kukua kwa soko la nyama la ndani na nje ya nchi,katika mwaka 2023/2024, jumla ya vifaranga vya kuku 95,584,347 vimezalishwa na kusambazwa nchini ikilinganishwa na jumla ya vifaranga 83,845,967 vilivyozalishwa mwaka 2022/2023, sawa na ongezeko la asilimia 12.3. Kati ya vifaranga hivyo, vifaranga vya kuku wa nyama ni 73,481,572; chotara 14,163,396; na kuku wa mayai 7,939,379; ikilinganisha na vifaranga vya kuku wa nyama 64,457,555; chotara 12,424,064 na kuku wa mayai 6,964,348 kwa mwaka 2022/23.
Waziri Ulega amebainisha kuwa uzalishaji wa mayai nchini umeongezeka kutoka mayai bilioni 5.50, mwaka 2022/2023 hadi mayai bilioni 6.41, mwaka 2023/2024, sawa na ongezeko la asilimia 16.55 Ongezeko hilo limesababishwa na kuimarika kwa vituo 28 vya kutotolesha vifaranga vya kuku vilivyopo nchini, mashamba 25 ya kuku wazazi, kuongezeka kwa ufugaji wa kuku wa mayai na hatua mbalimbali ambazo zimeendelea kucukuliwa za kudhibiti uingizaji holela wa vifaranga kutoka nje ya nchi.
Uzalishaji wa maziwa umeongezeka kutoka lita bilioni 3.60, mwaka 2022/2023, hadi kufikia lita bilioni 3.97, mwaka 2023/2024, sawa na ongezeko la asilimia 10.3 ambapo kati ya lita hizo, lita milioni 34.69 zimetokana na maziwa ya mbuzi na lita bilioni 3.93 zimetokana na maziwa ya ng’ombe ,aidha lita bilioni 2.64 zinatokana na ng’ombe wa asili na lita bilioni 1.30 zimetokana na ng’ombe wa maziwa walioboreshwa.
Usindikaji wa maziwa umeongezeka kutoka lita milioni 77.90, mwaka 2022/2023, hadi kufikia lita milioni 81.80, mwaka 2023/2024, sawa na ongezeko la asilimia 5. pia, ukusanyaji wa maziwa kupitia vituo vya kukusanyia maziwa, umeongezeka kutoka lita milioni 71.80, mwaka 2022/2023, hadi kufikia lita milioni 93.40, mwaka 2023/2024.
Ongezeko la uzalishaji wa maziwa limechangiwa na utoaji elimu ya ufugaji bora wa ng’ombe wa maziwa kibiashara hapa nchini, kuongezeka kwa ng’ombe wa maziwa walioboreshwa pamoja na vituo vya kukusanyia maziwa vilivyofikia 258 mwaka 2023/2024 kutoka 246 mwaka 2022/2023.