Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Malu Stonch afariki dunia baada ya kuangyka jukwaani

Msanii mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Malu Stonch amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa kwenye majukumu yake ya kikazi.

Malu alianguka ghafla jukwaani katika ukumbi wa Target uliopo Mbezi Beach wakati akiimba pamoja na bendi yake anayofanya nayo kazi muda mrefu ya FM Academia.

Kiongozi wa FM Academia, Patcho Mwamba amesema, mwanamuziki huyo wakati anaimba alidondoka ghafla na kuangukia uso na kupoteza fahamu huku damu zikimtoka masikioni na kung’ata ulimi ndipo wakampa huduma ya kwanza kabla ya kumuwaisha Hospitali ya Masana.


Patcho amesema Malu alipopelekwa Masana walipompokea tu, wakaambiwa wamuwahishe Hospitali ya Lugalo kwa kuwa mgonjwa ameshafariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *