Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Madaktari waliokimbia kisa Baridi kusakwa

Serikali imesema itafuatilia madaktari ambao walipatiwa ajira na kupangiwa kituo cha kazi wilayani Ludewa mkoani njombe kisha kufanyiwa uhamisho kabla hata ya kuripoti wilayani humo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Festo Dugange wakati akijibu swali la nyongeza kutoka kwa mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga lilihoji juu ya mpango wa serikali katika kuziba nafasi za madaktari hao ambao hawakuripoti.

Aidha Waziri Dugange amesema mfumo wa sasa wa uombaji ajira ni wahitaji wanaomba moja kwa moja katika kituo husika na wanapopatiwa ajira hizo hawatakiwi kuomba uhamisho kwa kipindi cha miaka mitatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *