MACHINGA KARIAKOO WASISITIZWA UFUNGUAJI NJIA KURUHUSU BIASHARA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametoa wiki mbili kwa Uongozi wa Wafanyabiashara Wadogo maarufu kama Machinga wa Kariakoo, kuanza kufungua njia ili kuruhushu shughuli za kibiashara kufanyika kwa ufanisi wakati serikali ikielekea kufanya uzinduzi wa soko jipya.

Chalamila ameyasema hayo jijini Dar es Salaam na kudai kuwa wakati maandalizi ya uzinduzi wa soko jipya yakiendelea, ni muhimu Machinga wakafungua njia za kuingia, ili kupeleka bidhaa kwenye soko jipya la Kariakoo.

Amesema, “Soko limeshakamilika kwa asilimia 98 hivyo natoa muda wa wiki mbili kuanzia leo Mei 28,2025 Machinga waliopo barabarani Kariakoo wakaondoka kwenda maeneo waliyopangiwa.”

Akiwazungumzia Wafanyabiashara waliokuwepo kwenye Soko la Kariakoo awali kabla halijaungua, Chalamila amesema wote watahakikiwa na kurejeshwa kama ilivyoelekezwa na Rais Samia kwa kutlfuata utaratibu uliowekwa, ikiwemo kujaza mikataba, kulipa kodi kwani Mkoa umefanikiwa kuondoa udalali wa upangishaji maeneo kwa kutuia mfumo wa kidijitali wa TAUSI.

Awali, Meneja Mkuu Shirika la Masoko Kariakoo, Ashraph Abdulkarim alisema wanaendelea kuratibu wafanyabiashara waliokuwepo kurejea kwenye Soko hilo kulingana na mpangilio wa biashara.

Amesema idadi ya wafanyabiashara 1150 kati ya 1520 waliohakikiwa tayari wamesajiliwa kwenye mfumo wa TAUSI, ili kurejea sokoni na kuwa maeneo mengine ya wazi yaliyobaki yatatangazwa ili kuoata wapangaji wapya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *