WAUGUZI WAASWA KUTUNZA SIRI ZA WAGONJWA NA KUZINGATIA MAADILI

Na Saulo Stephen – Singida.

Wauguzi Mkoani Singida, wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao kwa kutunza siri za wagonjwa ikiwa ni pamoja kujiepusha na tabia zinazofedhehesha taaluma yao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Singida, JoanFeith Kataraiya wakati akimuwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatuma Mganga kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi ambapo katika mkoa wa Singida yameadhimishwa leo mei 30, kutokana na watumishi wengi wa mkoa huo kuhudhuria maadhimisho ya kitaifa yaliyofanyika mei 12 mwaka huu mkoani Iringa.

Amesema kumekuwepo na tabia kwa baadhi ya wauguzi kufanya vitendo visivyofaa na vinavyozalilisha taaluma hiyo muhimu, hivyo wanapaswa kubadilika na kufanya kazi kwa weledi pindi wawapo kazini lakini pia kuwa na tabia njema nje ya kazi ili kuwa mfano wa kuingwa kwenye jamii inayowazunguka.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Victorina Ludovic, akizungumza katika maadhimisho hayo amesema lengo kubwa la maadhimisho hayo ni kumuenzi muuguzu Frolence Nightngale ambae alifanya kazi ya uuguzi kwa moyo wa kujitoa na kuipenda kazi yake, hivyo amewaasa wauguzi mkoani Singida kumuenzi Nightingale kwa vitendo.

Nao baadhi ya wauguzi wa mkoa wa Singida wameiambia jambo fm, mara baada ya maadhimisho hayo kuwa watahakikisha wanaendelea kuitunza,kuilinda na kuiheshimisha taaluma ya uuguzi kwa kuwahudumia wagonjwa kwa weledi na kiwango cha hali ya juu kutokana na taaluma yao.

One response to “WAUGUZI WAASWA KUTUNZA SIRI ZA WAGONJWA NA KUZINGATIA MAADILI”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *