Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kwa Tanzania maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) yamepungua kutoka asilimia 7 mwaka 2003/2004 hadi kufikia asilimia 4.4 mwaka 2022/2023, kukiwa na tofauti kati ya watu na maeneo mbalimbali ya kijiografia.
Waziri Ummy amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa mapitio ya kimkakati wa PEPFAR COP muhula wa 23 kwa lengo la kutathmini hatua iliyofikiwa kuhusu mwitikio wa VVU katika kufikia udhibiti wa UKIMWI ifikapo mwaka 2030.