Katibu tawala wa wilaya ya Misungi Bw. Abdi Makange amewataka watumishi wote wa serikali waliopo ndani ya wilaya hiyo kutimiza majukumu yao kwa wakati kwani endapo atabainika mtumishi yoyote ambae ameshindwa kutimiza majukumu yake kwa wakati basi hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.
Makange ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa afya wa hospitali ya wilaya ya Misungwi ambapo amesema serikali ya wilaya hiyo haipo tayari kuona mwananchi yoyote anakosa huduma yoyote kwa wakati kwani kwa kiasi kikubwa suala hilo ndio limekua likisababisha kuwe na kundi kuwa la wananchi wanaotoa kero zao pale viongozi wakubwa wanapofika katika maeneo yao.