Staa wa muziki kutoka Nigeria, Davido anaendelea kumuenzi mtoto wake Ifeanyi kwa kutengeneza kidani cha almasi chenye mfanano wa sura ya kijana yake huyo aliyefariki mnamo Novemba 1, 2022 baada ya kuzama kwenye bwawa la kuogelea nyumbani kwake.
Ifeanyi ni mtoto wa Davido na Chioma Rowland, na baada ya ajali hiyo ya kupoteza mtoto, wawili hao walifunga ndoa ya kimila na mwaka huu wamebarikiwa kupata watoto mapacha.