Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Kiwanda cha kutengeneza Biskuti za bangi chagunduliwa Dar

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imekamata kilo 423.54 za bangi iliyosindikwa maarufu kama Skanka huku pia kubaini uwepo wa kiwanda cha kutengeneza biskuti zilizochanganywa na bangi katika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Novemba 8, 2023 jijini Dar es Salaam Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema wamekamata Skanka baada ya kufanyika operesheni maalum zilizofanyika kwenye mipaka na fukwe za Bahari ya Hindi.

Amefafanua kilo 158.54 zilikamatwa eneo la Kigamboni na Kawe jijini Dar es Salaam zikiwa zimehifadhiwa ndani ya mabegi ya nguo tayari kwa kusafirishwa, kilo 265 zilikamatwa katika matukio tofauti mikoa ya nyanda za juu Kusini zikiwa zimefichwa ndani ya magari kwa kuchanganywa na bidhaa nyingine ikiwemo maboksi yenye matunda aina ya Apples zikisafirishwa kuelekea jijini Dar es Salaam.

Pia amesema Mamlaka hiyo imekamata watu wanaojihusisha na utengenezaji wa biskuti kwa kuchanganya na Skanka katika eneo la Kawe huku akifafanua katika tukio hilo watuhumiwa walikutwa wakiendelea na uzalishaji wa biskuti hizo kwa kutumia mtambo mdogo wa kusaga skanka na vifaa vya kutengeneza biskuti za bangi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *