
Newcastle, Chelsea na Liverpool zote zimeonesha nia ya kumsajili beki wa Sporting mwenye umri wa miaka 20 Ousmane Diomande.
Katika Msimu wa 2022|2023 mchezaji huyo alihusishwa na klabu za Manchester City, Arsenal na Southampton kutokana na kipaji cha pekee alichonacho beki huyo wa kati ambaye alisajiliwa na Sporting CP kwa Euro milioni 7.5, na kumfanya kuwa mchezaji wa pili kusajiliwa kwa gharama kubwa msimu wa baridi katika dirisha la uhamisho nchini Ureno (nyuma ya Andreas Schjelderup wa Benfica).
Diomande alianza kucheza soka katika klabu ya Olympic Sport Abobo nchini Côte d’Ivoire. Na baada ya kufaulu huko, alijiunga na kikosi cha Midtjylland na kuitumikia timu yao ya vijana wenye umri chini ya miaka 19 ambayo aliichezea katika Ligi ya Vijana ya UEFA na tayari na kuonesha uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya beki wa kushoto na kulia wakati huo huo akiimudu nafasi ya beki wa kati.