Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Kifo cha mama na mtoto, 6 wasimamishwa kazi Kahama

Serikali imewasimamisha kazi watumishi sita wa hospitali Ya wilaya ya kahama mkoani Shinyanga baada ya kutokea tukio la kupoteza maisha kwa mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Rachel Wiliam na kichanga chake, kwa kukosa huduma katika hospitali hiyo alipofika kwa ajili ya kujifungua na kunyimwa huduma baada ya kukosa fedha.

Akizungumza na Jambo Fm kuhusiana na tukio hilo Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita amesema serikali haipo tayari kuona watu wachache wanaharibu sifa ya serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati ikiwa ni pamoja wananchi kupewa kipaumbele katika suala la matibabu.

Akizungumzia tukio hilo kiongozi wa familia ya binti aliyepoteza maisha mwana Mbalu Shinje ambaye baada ya tukio hilo alisusia kuchukua miili hiyo ajili ya mazishi amesema kitendo hicho ni cha kinyama na na kuongeza kuwa kimeacha simanzi kubwa katika familia hiyo huku akiiomba serikali kuwachukulia hatua stahiki wale wote waliohusika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *