
Waumini Wa Dini Ya Kiislamu Mkoani Shinyanga Wametakiwa Kusheherekea Sikukuu Ya Kuchinja Eid Al-Adha Kwa Kusaidia Watu Wenye Uhitaji Ili Kupata Thawabu Kwa Mwenyezi Mungu.
Sheikh Wa Mkoa Wa Shinyanga, Ismail Mkusanya Amebainisha Hayo Leo Wakati Akiongoza Swala Ya Sikukuu Ya Kuchinja Eid Al-Adha Katika Viwanja Vya Sabasaba Manispaa Ya Shinyanga.
Amesema Katika Kusherehekea Sikukuu Hiyo Ya Kuchinja Ni Vyema Waumini Wa Dini Hiyo Wakafurahi Pamoja Na Watu Wenye Uhitaji Wakiwamo Yatima, Wajane, Wafungwa,Wazee, Watoto Wenye Ualbino, Na Majirani Kwa Kula Nayo Chakula, Na Siyo Kuifanya Siku Hiyo Kuwa Ya Anasa.
“Ndugu Zangu Waislamu Jengeni Utamaduni Wa Kusaidia Watu Wenye Uhitaji Na Sikukuu Hii Ya Kuchinja Tuwaite Tule Nao Chakula Cha Pamoja Na Kujiongezea Thawabu Kwa Mungu,” Amesema Sheikh Makusanya.