Mkuu wa Jeshi la Polisi chini, IGP Camillus Wambura amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe na Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar.
Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Martin Otieno aliyehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma.
Uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Polisi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.