
Muigizaji,Mwanamitandao na staa kutoka Ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amekuwa Mtanzania pekee aliyeshiriki na kunogesha ujio mpya wa tamthiliya ya Bridgerton, katika onesho kabambe lililowakusanya nyota “A list” na daraja la kwanza kutoka Afrika Mashariki na Bara la Afrika kwa ujumla.
Onesho hilo lilifayika Mei 4, mwaka huu nchini Afrika Kusini ambapo Netflix ambao ndio waandaaji wa Series hiyo, walizindua msimu wa tatu wa Bridgerton,na Bridgerton ya msimu wa inatarajiwa kurushwa na Netflix na kushuhudiwa na ulimwengu mzima Mei 16, mwaka huu ambapo itaruka sehemu ya kwanza na sehemu ya pili itaachiwa Juni 13, mwaka huu.

Miongoni mwa Mastaa wengine waliohudhuria katika onesho hilo, lililopewa jina la ‘Regency Era Splendor: Into the Spotlight’ ni kutoka katika nchi za Kenya iliyowakilishwa na Catherine Kamau (Kate) na Elsa Majimbo,mataifa mengine yaliyokuwa na wawakilishi ni Nigeria, Ghana, Zimbabwe, Botswana na Afrika Kusini, wakiongozwa na Adjoa Andoh (ambaye amecheza kama Lady Aga kwenye Bridgerton) akiwa kama mgeni wa heshima.

Mpaka sasa Idris Sultan ndiye Mtanzania pekee mwenye mafanikio makubwa ya kisanaa aliyeweza kutoboa na kuwa na kazi kwenye mtandao wa Netflix kupitia filamu ya “Slay” kazi ambayo ilimfanya Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Kummwagia Pongezi akimuelezea kuwa ametuweka Watanzania kwenye uso wa Netflix.