Ibada Kufanyika kwa Saa 2, Kudhibiti Kipindupindu

Wakati wizara ya afya nchini ikiendelea kutoa tahadhari juu ya ugonjwa wa kipindupindu, na kuwasihi wananchi kuzingatia usafi, nchini Zambia hali ni mbaya Zaidi kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa walioambukizwa ugonjwa huo.

Zaidi ya Wagonjwa 7,800 wa Kipindupindu wameripotiwa nchini humo tangu Oktoba 2023, na kusababisha vifo vya watu 18, huku biashara za Vyakula ambavyo vimeshapikwa tayari imepigwa marufuku pamoja na Waumini kutakiwa kutosalimiana kwa kushikana Mikono ili kuepusha hatari ya kupata Maambukizi.

Halikadhalika Ibada zimetakiwa kufanyika kwa muda usiozidi Saa 2, agizo linalolenga kupunguza kuenea kwa Ugonjwa wa Kipindupindu nchini humo.

Tanzania ni kati ya Nchi za ukanda wa Afrika Mashariki zilizoripoti Maambukizi ya Ugonjwa huu kwenye Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Kagera, Tabora na Ruvuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *