Baadhi ya wananchi wameendelea kupuuzia kujenga vyoo katika makazi yao, na kupelekea kujisaidia kwenye vichaka hali ambayo inahatarisha usalama wa afya zao.
Katika mkoa wa simiyu oparesheni ya Wiki moja ya kukagua usafi wa Mazingira kwa Wananchi imebaini zaidi ya Kaya 70 kati ya 400 zilizokaguliwa hazina Vyoo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahaya Nawanda, amesema Kaya ambazo zimekutwa hazina Vyoo zimepigwa Faini na kutakiwa kujenga Vyoo haraka kwa kuwa hali hiyo ni chanzo cha mlipuko wa Magonjwa ya kuhara na kutapika.
Amesema baadhi ya Wananchi wanachukua kinyesi wanaweka kwenye Mifuko na kutupa Mtaani kwenye Mitaro, ndio maana mkoa huo umepata magonjwa ikiwemo Kipindupindu.