Imeelezwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanai Dkt Samia Suluhu Hassana amefanikiwa kuboresha sekta mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na afya elimu, majengo na miundomdombinu ambayo ni rafiki kwa kundi la watu wenye ulemavu ili kuhakikisha huduma hizo zinakuwa jumuishi pamoja na kundi hilo linaishi kwa kuheshimiwa katika jamii.
Hayo yameelezwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, Peres Kamugisha kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro katika ufunguzi wa Kongamano la watu wenye Walemavu Mkoani humo.
“Rais samia ameendelea kuboresha maeneo mbalimbali ukiangalia kwenye nyanja za afya tumeona huduma zinaboreshwa, majengo yanaboreshwa, miundombinu yote inaboreshwa ili kumfanya mtu mwenye ulevu kuitumia isiwe kinzani kwa mtu huyu mwenye ulemavu,” amesema Kamugisha.

Aidha Kamugisha amesema kundi hili la watu wenye ulemavu wana haki za kibinadamu ambazo wengine wanazipata ikiwa ni pamoja na kuheshimiwa na kupata huduma zote muhimu za kijamii za afya, elimu, uchumi nakadhalika.
“Hapo awali katika sera zilizopita ilikuwa kwamba mtu mwenye ulemavu ni mtu ambaye hawezi kufanya chochote hata mipango inapopangwa haimuangalii katika muktadha mwingine wa kiuchumi na kimaendeleo” amesema Kamugisha.
Vilevile Kamugisha ameeleza kwamba serikali imefanya kazi kubwa kwenye nyanja za uratibu wa mabaraza ya watu wenye ulemavu akitolea mfano baraza la taifa la watu wenye ulemavu yenye jukumu la kuhakikisha yanasimamia haki, wajibu na haki za watu wenye ulemavu pamoja na kutafsiri vyema katika jamii juu ya uwepo wao na mambo wanayoweza kufanya kama vile kuwania na kushika nafasi mbalimbali za uongozi.

Akizungumzia suala la elimu jumuishi Kamugisha amesema kwa sasa taifa linaelekea pazuri kwa kuanzisha elimu jumuishi katika shule mbalimbali ili kuwaweka pamoja na karibu watu wenye uleamavu ili kuweza kujifunza na kushirikiana nao na kuondoa dhana ya kutengwa katika Jamii inayowazunguka.
Hata hivyo, Kamugisha amelisihi kundi hilo la watu wenye ulemavu kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa na serikali kufanya shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato na kuondokana na tabia ya kuombaomba mtaani bila kuweka kando uaminifu wa kurejesha fedha hizo baada ya kuapatiwa ili kuwapa nafasi na wengine kupata mikopo hiyo.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko ametumia nafasi hiyo kuwasihi watu hao wenye ulemavu kutokaa nyuma bali kuchukua hatua ya kushiriki katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka huu kwa kuchagua kiongozi anayefaa na kuchaguliwa ili kuweza kuingia katika nafasi za maamuzi ambapo itakuwa rahisi kusikiliza,kuwakilisha na kutetea kundi lao kwa uhakika .
Baada ya kufunguliwa kwa Kongamano hilo zimewasilishwa mada kuu mbili kwa kundi hilo ya elimu ya ujasiliamali kwa lengo la kuwakwamua katika wimbi kubwa la utemezi pamoja na elimu ya mkopo na faida zake.