ZAIDI YA WATU 200 WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA NDEGE INDIA

Zaidi ya watu 200 wamefariki dunia kufuatia ajali ya Ndege ya Air India iliyoanguka muda mfupi baada ya kupaa katika mji wa magharibi mwa India wa Ahmedabad.

Tukio hilo limetokea hii leo Juni 12, 2025 na kurhibitishwa na Kamishna wa Polisi wa jiji hilo G.S. Malik ambaye amesema Ndege hiyo, ilikuwa na abiria 242 na wafanyakazi na ilianguka katika chuo cha matibabu takriban maili tatu na nusu kusini magharibi mwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sardar Vallabhbhai Patel.

Kamishna Malik, amesema Wafanyakazi wa dharura walipata miili 204 kutoka eneo la ajali, na hakuondoa uwezekano wa manusura huku miongoni mwa wakiwa ni Wanafunzi watano wa chuo cha matibabu.

Ndege hiyo inadaiwa iligonga chumba cha kulia Wanafunzi walipokuwa wakipata chakula cha mchana, taarifa ambayo ilitoleq na Mkuu wa chuo hicho, Minakshi Parikh

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *