Simba SC imesema itapeleka kikosi chake Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya watani, Yanga SC uliopangwa kuanza Saa 11:00 jioni.
Taarifa iliyotolewa jioni hii na Klabu hiyo imeeleza kuwa uamuzi huo unatokana ratiba iliyotolewa na Bodi la Ligi Nchini (TPBL), kuonesha mchezo huo utapigwa Juni 15, 2025 na haitakuwa tayari kucheza mechi hiyo tarehe nyingine.
Hata hivyo, mahasimu wao Yanga SC walishasisitiza mapema kuwa hawatocheza mchezo huo wakitoa sababu mbalimbali ikiwemo kudai ripoti ya sqbabi zilizopelekea mchezo hio kuahirishwa Machi 8, 2025.
