Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, akiwa Bungeni jijini Dodoma hii leo Juni 12, 2025 amesoma Bajeti Kuu ambapo amebainisha mambo muhimu ikiwemo suala la kupungua kwa umasikini Nchini, suala la kodi na deni la Serikali, ambapo hapa nimekuletea nukuu na mambo muhimu.
UMASIKINI.
“Tkwimu rasmi zinaonesha kuwa kati ya mwaka 1991 na 2018, umasikini umepungua. Mathalani katika kipindi hicho cha marejeo, asilimia ya watu waliokuwa wakiishi katika umasikini wa hali ya juu (umasikini wa chakula) ilipungua kwa kiasi kikubwa kutoka asilimia 21.6 hadi asilimia 8, huku kiwango cha umasikini wa mahitaji ya msingi kikishuka kutoka asilimia 38.6 hadi asilimia 26.4.”
DENI LA SERIKALI.
“Hadi Aprili 2025, deni la Serikali lilikuwa TZS trilioni 107.70. Kati ya kiasi hicho, deni la nje ni TZS trilioni 72.94 na deni la ndani ni TZS trilioni 34.76. Tathmini ya uhimilivu wa deni uliofanyika kwa mwaka 2024, ulionesha kuwa deni letu bado ni himilivu.”

MAPATO.
Kuhusu mapato, Dkt. Mwigulu amesema katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025, mapato ya ndani yalifikia shilingi trilioni 25.67, sawa na asilimia 100.2 ya lengo na ukuaji wa asilimia 16.5, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2023/24.
“Mapato yatokanayo na kodi ambayo yalichangia asilimia 82.7 ya makusanyo ya ndani yalifikia shilingi trilioni 21.2,” amessma Mwigulu.
KODI.
Aidha, amesema kwa mwaka 2025/2026 Serikali imepanga kusamehe kodi ya Ongezeko la thamani kwenye miamala ya ununuzi wa bima mtawanyo inayofanywa baina ya kampuni za bima Na zile za bima mtawanyo.
Waziri Mwigulu ameongeza kuwa lengo la hatua hiyo ni kuongeza ushindani wa kampuni za ndani, kukuza sekta ya bima Na kuhamasisha matumizi ya bima katika kukabiliana na majanga nchini.
UCHAGUZI MKUU.
“Nipende kuwafahamisha watanzania kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025 tutaugharamikia Kwa Fedha zetu wenyewe na zoezi hilo limekamilika,” amesema Dkt. Mwigulu.