GEITA YAPATA MABADILIKO YA KIUTAWALA MIPAKA YA MAJIMBO

Na Frank Aman – Geita.

Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza Mabadiliko Makubwa ya Kiutawala katika Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi Nchini ikiwemo Mkoa wa Geita ambapo yaliyoanzishwa katika hatua hiyo ni pamoja na Jimbo la Katoro lililobadilishwa mara baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Busanda, Chato Kusini lililobadilishwa baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Chato, Mkoani humo.

Taarifa iliyotolewa na NEC Leo hii imeelezwa Mabadiliko hayo katika Mikoa Mingine ikiwemo Jimbo la Solwa, Mkoani Shinyanga na Kivule mara baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Ukonga Mkoani Dar es Salaam ambapoTaarifa hiyo imeelezwa Majimbo hayo mapya  yamegawanywa kutoka na kuwa baadhi yake yalikuwa na idadi kubwa ya Wapiga Kura kutokana na ongezeko la Watu katika Maeneo hayo.

Pia mabadiliko hayo yamefanywa kwa Jimbo la Mtumba lilianzishwa baada ya kugawanywa kuwa jimbo la Dodoma Mjini, Mkoa wa Dodoma, Uyole lilianzishwa mara baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Mbeya Mjini, Mkoa wa Mbeya na Bariadi Mjini lililoanzishwa mara baada ya kugawanywa kwa Jimbo la Bariadi, Mkoa wa Simiyu.

Aidha Tume imesema Mabadiliko hayo ni sehemu ya maboresho ya Mipaka ya Kiutawala ili kuhakikisha uwiano wa idadi ya watu kwenye Majimbo ya Uchaguzi na nafasi ya uwakilishi wa Wananchi Bungeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *