Kamati ya maadili ya shirikisho la soka nchini Uganda (FUFA), imemfungia mwamuzi George Nkurunziza, kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu nchini humo kwa kipindi cha miaka 10, baada ya kukutwa na kosa la kupanga matokeo.
Pia, kamati ya maadili ya FUFA imewafungia wachezaji wawili wa klabu ya Gaddafi FC, Mahad Yaya Kakooza na Andrew Waiswa kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu nchini humo kwa kipindi cha miaka mitano kwa kosa hilohilo la kupanga matokeo.
Mwaka jana FUFA ilimfungia mwamuzi John Bosco Kalibala kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu nchini humo kwa kipindi cha miaka 15 kutokana na upangaji wa matokeo.
Mwaka huo pia FUFA iliwafungia Meneja wa Masoko na Mauzo wa klabu ya Polisi FC, Kocha James Kaweesa na mwandishi wa michezo David Isabirye kujihusisha na soka.