Simba yasajili kipa wa Far Rabat ya Morocco

Klabu ya Simba imetangaza kumsajili mlinda mlango Ayoub Lakred kutoka kwa Mabingwa wa Ligi Kuu Morocco, FAR Rabat inayonolewa na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Young Africans, Nasreddine Nabi.

Lakred (28) raia wa Morocco ambaye aliiongoza FAR Rabat kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Morocco sambamba na na kuifikisha nusu fainali ya kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita amesaini mkataba wa miaka miwili.

Lakred ana uzoefu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Simba inaamini atakuwa msaada mkubwa kwenye Michuano hiyo.

Lakred anakuja Simba kuungana na Ally Salim, Hussein Abeli na Ahmed Feruz kipindi hiki ambacho, Aishi Manula anaendelea kuuguza jeraha lake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *