Davido ampongeza Tyla kushinda Grammy

Licha ya kukosa tuzo ya Grammy, usiku wa kuamkia leo, Staa wa muziki kutoka Nigeria Davido amempongeza mwandada Tyla kutoka Afrika Kusini kwa kushinda Tuzo ya “Best African Music Performance” kupitia wimbo wake Water

 Davido amempongeza mrembo huyo mwenye miaka 22 kupitia ukurasa wake wa Twitter(X).

Mbali na hivyo Davido amekosa Tuzo, lich aya kutajwa kuwania vipengele Vitatu ambavyo ni- Best Global Music Album (Timeless), Best Global Music Performance (Feel, Unavailable) na Best African Music Performance.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *