Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Burna Boy alipia bango kuweka wakina mama wa sokoni

Staa wa muziki Burna Boy ameamua kulipia bango (Billboard) huko soko la Makola – Ghana na kuweka picha za wakina mama waliokuwa wakicheza wimbo wake City Boy unaopatikana kwenye albamu yake ya I TOLD THEM

Ipo hivi.. baada ya wakina mama hao kushoot video wakicheza wimbo huo na video kuwekwa mtandaoni na kijana Raja, ambaye amekuwa akitengeneza maudhui ya wakina na mama wa soko hilo wakicheza muziki.

Basi akapost na kum-tag Burna Boy ambaye ali-like picha hiyo, kisha baadae group la Team Burna Boy wakashare link ya video hiyo… ooh ikawa ‘No problem’ uongozi ukalipia gharama za kuweka tangazo kwenye billboard ya Makola na ukaweka picha ya wakina mama hao na huku ujumbe wake ukiwa ni “Upendo kutoka sokoni kwa wakina mama hawa, kutoka mji wa furaha”.

Kibongo bongo unadhani zile challenges zinazofanya na watu kwenye ngoma za mastaa unadhani ipo siku watawekwa kwenye bango?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *