Orodha ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha la Tamaduni nchini Uganda maarufu kama Nyege Nyege Festival wametajwa ambapo kuna Sho Madjozi, Eddy Kenzo, A Pass, Janzi Band & Karole Kasita, Mejja Genge na Trio Mio.
Tamasha hilo litafanyika kuanzia Novemba 9-12 na litajumuisha mataifa kama Tanzania, Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Mali, Malawi, Cameroon, Ghana, Rwanda, Algeria, Sudan Kusini, Angola, Mauritius, Saint Lucia, DR Congo, Finland, Marekani, Ufaransa, Japan na Ujerumani .