BALOZI JUMA MWAPACHU AFARIKI DUNIA

Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Afrika Mashariki – EAC, (2006-2011), Balozi Juma Volter Mwapachu amefariki dunia.

Balozi Mwapachu amefariki Machi 28, 2025 jijini Dar es Salaam, na taarifa zaidi juu ya ki for chake bado hazijabainishwa.

Enzi za uhai wake, Mwapachu amewahi kushika nyadhifa mbalimbali, ikiwemo Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa.

Itakumbukwa pia Balozi Mwapachu alijitoa CCM Oktoba 2015, kuunga mkono upinzani na juhudi za aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Nchini, Edward Lowassa na baadaye mwaka 2016 alirirrjea tena.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *