MVUA ZAATHIRI USAFIRI WA MWENDO KASI, NJIA ZAFUNGWA

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, zimepelekea Kampuni ya Mabasi yaendayo Haraka (UDART), kusitisha huduma za usafiri za Mbezi/Kimara – Gerezani na Kivukoni.

Taarifa ya UDART imeeleza kuwa itaendelwa na huduma za Mbezi/ Kimara – Magomeni Mapipa na Kimara kwenda Morocco, Mbezi, Mlonganzila na stendi ya Magufuli.

Sitisho hilo linatokana na mkondo wa maji wa Mto Msimbazi kuathiri matumizi ya Barabara katika eneo la Jangwani na kupelekea kufungwa kwa Barabara ya Magomeni Mapipa – Fire katika eneo la Daraja la Jangwani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *