Staa wa muziki, Alikiba ameweka wazi kuwa yeye ndio alimshawishi Nandy kufanya naye remix ya ‘Dah’.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2024/02/Snapinsta.app_425472544_18416605156035011_382396090169045854_n_1080-1-821x1024.webp)
Alikiba amefunguka hayo kupitia mahojiano aliyofanya kupitia Power Fresh ya Jambo FM hivi karibuni
“Ni mimi ndio nilimshawishi Nandy, Na approaching yangu siku zote inakuwaga kwa kupiga stori ila nilianza kwa kumpa hongera ya nyimbo yake. Na nilimwambia verse ya kwanza ni kali kama imefunika Verse ya Pili, ndio akasema dah hata mimi naona, Nandy akasema basi tufanye ndio akaja Ofisini kwangu tukafanya kazi baada ya hapo wakachukua na kwenda kufanya Mixing na vitu vingine nje ya Studio za Kings,” amefunguka Alikiba.