Alifariki kwa uzembe wa wauguzi na sio kukosa Tshs. 150, 000/-

Tume iliyoundwa na Waziri wa afya, Ummy Mwalimu kuchunguza kifo Cha mjamzito, Marium Zahoro imebaini kuwa kifo hicho kilitokana na uzembe wa wataalamu wa afya na sio kutokana na kukosa fedha za matibabu kiasi cha Sh. 150,000.

Akiongea katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kituo cha afya cha Kabuku, Waziri Ummy amesema kuwa tayari baraza la madktari pamoja na waguuzi na wakunga linaendelea na utaratibu wa kuchukuwa hatua za kinidhamu kwa wataalamu wawili wa afya katika kituo hicho.

Kifo cha Marium Zahoro kilitokea mnamo Novemba 11 katika kituo cha afya cha Kabuku baada ya kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida na kuhitaji kufanyiwa upasuaji na kuchelewa kwa huduma ya dharura ya upasuaji.

Aidha akiwasilisha taarifa ya tume hiyo , Mwenyekiti wa tume Dkt Ali Said amesema kuwa chanzo cha kifo cha Marium ni kutokana na uzembe wa wataalamu hao kushindwa kuchukuwa hatua za haraka ili hali mgonjwa akiwa katika hali ya hatari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *