Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya
uteuzi wa viongozi mbalimbali, ambapo Dkt. Ismael Aaron Kimirei ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI), kwa kipindi cha pili;
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka imeeleza kuwa Balozi Ernest Jumbe Mangu, naye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kipindi cha pili.

Aidha, Dkt. Marina Alois Njelekela. ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), akichukua nafasi ya Prof. Charles Mkony ambaye amemaliza muda wake.
Rais Samia pia amemteuwa Juma Hassan Fimbo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na
Prof. James Epiphan Mdoe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya
Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), akichukua nafasi ya Dkt. Andrew Kitua ambaye amemaliza muda wake.
