Rapa Kanye West ametangaza kuwa albamu yake mpya iitwayo ‘Vultures’ yenye ngoma zipatazo 17 na itatoka Ijumaa hii Disemba 15.

Listening party ya albamu hiyo imefanyika usiku wa kuamkila leo na imeudhuriwa na mastaa kama Ty Dolla $ign, Offset, Chris Brwon, Kodak Black, Lil Drunk na Binti yake North West ambaye anatajwa kushiriki kwenye albamu hiyo.

Pia katika albamu hii kuna ngoma iitwayo ‘New Body’, ambayo imesubiriwa kwa muda mrefu inayomjumuisha mwanadada Nicki Minaj.