Mwanamke mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Devotha Gilbert (20), mfanyabiashara na mkazi wa Kata Mwembesongo mkoani Morogoro, anadaiwa kuuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali mwilini na mumewe, kisha mwili kutelekezwa katika eneo la Mafisa kwa Mambi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Desemba 12, 2023, ambapo chanzo kinadaiwa ni mgogoro wa kifamilia na wivu wa kimapenzi.
Kamanda Mkama, amemtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo ni mumewe aliyetambuliwa kwa jina la Boniface John (26) mfanyabiashara wa Machinjio na mkazi wa Kata ya Kichangani, Manispaa ya Morogoro.
Amesema baada ya kutekeleza mauaji ya mkewe, mtuhumiwa hiyo aliondoka akiwa na pikipiki yake yenye namba za usajili MC 711 CQV aina ya Houjue na kuelekea mtaa wa Kindibwa, kata ya Bigwa ambapo aliamua kujiua mwenywe kwa kujichoma kisu shingoni na tumboni.