Mahakama Kuu ya Afrika imemhukumu Johannes Ontsheketse Tshabile(43), kifungo cha maisha 11 kwa tuhuma za ubakaji.
Pia imemuhukumu kifungo cha miaka 363 kwa makosa mengine 9 ya ubakaji, jaribio la kuua, wizi, ujambazi wa silaha, kudhuru mwili, kujaribu kutenda kosa la ngono na unyanyasaji wa kijinsia amebainisha hayo Msemaji wa Mamlaka ya Mashtaka ya Taifa (NPA) Kanda ya Kaskazini Magharibi, Henry Mamothame, katika taarifa yake aliyotoa siku ya jana Ijumaa Februari 23, 2024.