Mkaguzi Msaidizi wa polisi Getruda S. Mwiga amewataka wananchi wa kata ya Nyaruzumbura wilaya ya Kyerwa mkoa wa Kagera kuacha tabia ya kunywa pombe kali kupita kiasi hadi kupelekea kifo.
Mwiga ametoa rai hiyo wakati aliposhiriki kwenye tukio la mazishi ya mtu mmoja aliyefariki dunia kutokana na kunywa pombe kupita kiasi wakati wa sikukuu ya Krismass.