Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Dc Samizi awa mbogo,atoa maagizo Shinyanga Dc

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi ameagiza uboreshwaji wa ukusanyaji wa mapato kutokana na halmashauri hiyo kuwa chini ya asilimia 50 ya ukusanyaji wa mapato hali aliyoelezea kuwa ni mbaya na kuagiza kuwasilishwa kwa orodha ya wawekezaji wote wanaoendesha shughuli za uchimbaji wa madini katika ofisi yake ijumaa ya Machi 8 mwaka huu.

Ameyasema hayo kupitia kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya  wilaya hiyo kilichoketi Machi 6 mwaka huu na kutumia fursa hiyo kuwataka madiwani kuhakikisha wanadai risiti halali za kielektroniki pindi wanaponunua bidhaa au kupatiwa huduma hatua itakayowezesha kuzuia upotevu wa mapato ya serikali yanayopaswa kutumika katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.

“Haiwezekani tunaambiwa tubuni vyanzo vya mapato,wawekezaji wanakuja halafu kuna mtu anajiona yuko honey moon wakati wengine wanahangaika yeye anakula maisha,kufikia ijumaa hii nipate orodha ya wawekezaji wote mezani kwangu”amesema Dc Samizi.

Aidha amebainisha uwepoa wa baadhi ya madiwani ndani ya halamshauri hiyo ambao wamekuwa na tabia ya kutojishughulisha na suala la ukusanyaji wa mapato na baadhi ya maeneo wamekuwa wakiwasaidia wanaotorosha mapato na baadae kulalamikia kusimama kwa miradi ya maendeleo katika kata zao na kumuagiza mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuwakamata madiwani hao.

Awali wakiwasilisha hoja kuhusiana na utambuzi wa wawekezaji wanaofanya shughuli za uchimbaji wa madini katika kata ya Mwakitolyo diwani wa kata ya Ilola Amosy Mshandete,diwani wa kata ya Salawe Joseph Buyugu na Masalu Nyese ambaye ni diwani wa kata ya Mwakitolyo wameelezea kushangazwa na watendaji kutofanyia kazi agizo la baraza lililohusu uainishaji wa wawekezaji katika sekta ya madini hali ambayo ingewezesha upatikanaji wa mapato.

Kufuatia uwepo wa kile kinachoonekana kuwa ni uzembe kwa watumishi waliohusiaka kuchukua orodha ya wawekezaji wanaofanya shughuli za uchimbaji wa madini katika kata ya Mwakitolyo na kutoyawasilisha katika ofisi ya mkurugenzi,mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngasa Mboje amemuagiza Mkurugenzi wa wilaya hiyo Kisena Mabuba kueleza hatua alizozichukua kwa wahusika wa uzembe huo kupitia kikao cha baraza la madiwani kinachotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *