Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mwanafunzi auawa kwa kuchinjwa baada ya kudanganywa atapewa zambarau

Mwenyekiti wa kijiji cha Mapea Filmon Mbogo, amekiri kutokea kwa tukio la Mwanafuzi wa Chekechea mwenye umri wa miaka saba kuuwa kwa kuchinjwa na mtu asiyejulikana katika kijiji cha Mapea kata ya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara,  Feb 20 Mwaka 2024 na kusema baada ya kupata taarifa hizo ameliarifu jeshi la polisi ili kupata maelekezo kuhusu mwili huo.


Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mapema wamesema mtoto huyo alikuwa anasoma katika shule ya msingi Mapea, na wakati wakitoka shule walikutana na mtu wasiomfahamu ambaye aliwadanganya anakwenda kuwachumia mazambarau ambapo alimchukua mtoto huyo na kwenda kumchinja shambani kwa kumtenganisha kichwa na kiwiliwili.


Aidha, kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara, George Katabazi amethibitisha kutokea kwa tukio nakusema atatolea ufafanuzi baada ya kupata taarifa kamili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *