Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Radi yaua watatu na kujeruhi 19 wakiwa kwenye matanga

Watu watatu wamefariki dunia na wengine 19 kujeruhiwa kwa kupigwa na Radi wakiwa kwenye Matanga katika Kijiji cha Nahukahuka Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi, jana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema kuwa tukio hilo limetokea katika kijiji hicho ambapo watu hao walikuwa kwenye Matanga ya Msiba.


Mganga Mfawidhi, Dokta Abdallah Mputa wa Kituo cha Afya, Nyangamara amekiri kupokea miili ya marehemu hao na majeruhi 19 waliofikishwa hospitalini hapo jana hiyo hiyo.

mesema kati ya majeruhi 19 waliopokelewa kituoni hapo 13 wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa kurejea nyumbani, huku majeruhi 6 wakiendelea kupatiwa matibabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *