Aliyeua watu 13 na kuwazika jikoni kwake ahukumiwa maisha jela

Mahakama imemuhukumu kifungo cha maisha Gerezani Denis Kazungu na faini ya milioni kumi Mshukiwa wa mauaji ya watu 13 nchini Rwanda.


Denis Kazungu anashutumiwa kwa makosa kumi likiwemo la kuwazika watu 13 katika shimo alilokuwa amelichimba ndani ya nyumba aliyokuwa anaishi.



Kazungu akiwa mbele ya Mahakama ya Nyarugenge amekiri kuhusika katika mauaji ya waschana 12 na Mvulana mmoja na kuwatupa katika shimo hilo kwa nyakati tofauti.


Amesema kuwa hata yeye hajui sababu ya kutenda uovu huo wa kati ya mwaka wa 2022-2023 huku akiiomba Mahakama kumpunguzia adhabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *