Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wakazi wa Gaza wala chakula cha mifugo kujinusuru na njaa

Wakazi wa maeneo ya kaskazini mwa Gaza wamelalamika   kukosa chakula kwa siku kadhaa sasa, huku misafara ya misaada ikizidi kunyimwa vibali kuingia eneo hilo, na kusababisha baadhi ya wakazi kusaga chakula cha mifugo kuwa unga ili kujipatia chakula wakati akiba ya nafaka hizo inapungua.

Wakazi hao wamesema wanachimba kwenye udongo ili kupata mabomba ya maji ya kunywa kutokana na uhaba wa maji uliopo gaza,ambapo umoja wa mataifa (UN) umeonya kwamba, utapiamlo mkali miongoni mwa watoto wadogo kaskazini mwa Gaza umeongezeka kwa kasi.


Shirika la umoja wa mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu (OCHA), limesema zaidi ya nusu ya misaada kaskazini mwa Gaza ilikatazwa kufika mwezi uliopita, huku ikikadiriwa zaidi ya watu 300,000 wanaoishi katika maeneo ya kaskazini kwa kiasi kikubwa wamesitishiwa msaada.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *