Mkazi wa Kijiji cha Mtimbwilimbwi katika Halmashauri ya Mji wa Nanyamba, mkoani Mtwara, Dadi Linyata amefariki dunia kwa kupigwa na radi akitokea msibani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuwasihi wananchi kuendelea kuchukua tahadhari hasa kipindi hiki cha mvua.