Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Jina Pele laingizwa katika kamusi maalumu ya Kireno

Jina la utani la aliyekuwa gwiji wa soka duniani, Edson Arantes do Nascimento (Pele) limeingizwa rasmi kwenye kamusi likimaanisha kitu au jambo la “kipekee, kisicholinganishwa”.

Kamusi ya Michaelis ya lugha ya Kireno, ni moja ya kamusi maarufu zaidi nchini Brazil, iliongeza neno “Pele” kama kivumishi kipya ambapo kuingizwa kwa jina lake kwenye kamusi hiyo kulikuja baada ya kampeni ya Pelé Foundation ya kumuenzi nyota huyo wa kandanda kukusanya saini zaidi ya 125,000.

Pele alifariki mwezi Disemba, 2022 akiwa na umri wa miaka 82 na ndiye gwiji wa soka pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu, anachukuliwa kuwa mwanasoka bora zaidi kuwahi kutokea duniani, Katika historia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *