Nabii kutoka Nigeria, Adetoun Onajobi amedai kuwa Marehemu Mohbad atatokea na kushi kwenye familia nyingine baada ya miaka mitatu.
Nabii huyo amesema hayo katika mahojiano ya hivi karibuni kupitia Oyinmomo Tv, ambapo alisisitiza kuwa kwa sasa roho ya Mohbad iko mahali ikiwa imefumzika.
Adetoun amedai kuwa marehemu alimwendea mwanamke mjamzito ili aweze kuishi katika mwili wake na kuzaliwa upya lakini mwanamke huyo alikataa.
Alidai kuwa Mohbad angezaliwa upya katika familia nyingine katika miaka mitatu ijayo.
“Mohbad sasa yuko mahali pake pa kupumzika. Alikwenda kukutana na mwanamke mjamzito na kumwomba aingie ndani ya mwili wake. Mwanamke mjamzito alikimbia na kukataa. Nenda kaandike, katika muda wa miaka mitatu, Mohbad ataingia tena katika familia nyingine na si katika familia ya baba au mama yake.”
Moh bad amefariki Septemba 12, mwaka huu huko nchini Nigeria na kifo chake kimeendelea kuzua utata kutokana na taafifa mbalimbali ya chanzo cha kifo.