Mradi uliotumia milioni 702 waondoka na watatu

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Said Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi watatu na kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili ikiwemo kuongeza gharama za ujenzi wa miradi ya halmashauri kutoka Sh milioni 584.2 hadi kufika Sh milioni 702 tofauti na maelekezo.

Akiongea mara baada ya kukagua ujenzi wa shule ya sekondari ya Kiomoni ambayo inajengwa kupitia mradi wa SEQUIP amesema kuwa watumishi hao wamekiuka na kuongeza gharama za ujenzi na kusababisha mradi kutokamilika kwa wakati.

Amesema kuwa serikali ilitoa kiasi cha sh milioni 584.2 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo mpya ya kata lakini kutokana na kuongeza gharama za ujenzi huo umepelekea hadi gharama za ujenzi kuongezeka na kufikia Sh milioni 702.

Ameyataja majengo mengine ambayo yalitakiwa yajengwe kwenye mradi huo lakini hayajengwa kuwa ni maktaba, chumba cha Tehama pamoja na matundu ya vyoo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *