Serikali kuwaadhibu wanajeshi walioua watu 85 kwa bahati mbaya

Serikali ya Nigeria imesema itawaadhibu Wanajeshi waliohusika na shambulizi kwa kutumia Ndege zisizo na Rubani na kuua takriban Raia 85 kimakosa Desemba 3, 2023, huku Wanaharakati Nchini humo wakizidisha shinikizo la kufanyika Uchunguzi.

Jeshi la nchi hiyo limesema Wanajeshi hao walikuwa wakifanya doria za Anga walipoona kundi la Watu waliokuwa kwenye Sherehe katika Kijiji cha Tudunbiri, Kaskazini Magharibi mwa Jimbo la Kaduna walitafsiri kuwa ni Wanamgambo, ambapo Ndege isiyo na rubani iliwashambulia na kuua watu 85, huku 66 wakijeruhiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *