Leo Desemba 8, 2023 Watumiaji wa huduma za Usafiri za Mabasi ya Masafa Marefu (Mabasi ya Mikoani) na Mafupi (Daladala) wanakutana na gharama mpya za Nauli.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini LATRA, nauli za Mabasi yote zimepanda baada ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya Watoa Huduma na Wadau wa Usafiri (Wananchi).