Staa wa muziki kutoka Afrika Kusini, Tyla ameweka wazi kuwa yupo mbioni kuachia albamu yake ya kwanza ifikapo 2024.
Mrembo huyo amefunguka hayo kupitia kipindi cha “COLORS” ambapo aliimba ngoma yake mpya iitwayo “On and On”.
Katika ukurusa wake wa X, amewataka mashabiki zake kuanza kuoda albamu yake hiyo ambayo ameandaa kwa takribani miaka miwili na ameipa jina la ‘Tygers’.